1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yaimarisha usalama kwenye mpaka wake na DRC

18 Januari 2023

Uganda imepeleka wanajeshi kwenye mpaka wa Mpondwe baina yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya shambulizi la kigaidi kwenye kanisa ambalo liliuwa watu 17 na kuwajeruhi wengine katika mji wa Kasindi nchini.

https://p.dw.com/p/4MLz0
DR Kongo Grenzübergang Bunagana zu Uganda
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Uganda imepeleka wanajeshi kwenye mpaka wa Mpondwe baina yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya shambulizi la kigaidi kwenye kanisa ambalo liliuwa watu 17 na kuwajeruhi wengine dazeni kadhaa katika mji wa Kasindi nchini Kongo tarehe 15 mwezi huu.

Mkuu wa wilaya ya Kasese inayopakana na Kongo, Joe Walusimbi amesema wanajeshi hao wanachunguza mienendo ya waasi wa ADF wanaotaka kuvuka mpaka, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya gazeti la The Monitor linalochapishwa nchini Uganda.

Aidha, msemaji wa polisi ya Uganda Fred Enanga ameelezea kuwepo kwa operesheni za usiku zenye kuleta mashaka, za meli za mizigo na abiria katika ziwa Albert. Mwezi uliopita Uganda iliwakamata watu kadhaa wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa ADF, waliovuka mpaka na kuingia katika wilaya ya magharibi ya Ntoroko.