1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yafunga mpaka na Kongo

Leyla Ndinda14 Novemba 2012

Serikali ya Uganda imeufunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambao umekuwa ukiwanufaisha sana waasi wa M23 kwa kuyatoza kodi magari yanayoingia Kongo kutoka Uganda na nchi nyingine za Afrika mashariki.

https://p.dw.com/p/16ixp
Raia wa Kongo wakikimbia mapigano kati ya waasi wa M23 na serikali ya Kongo.
Raia wa Kongo wakikimbia mapigano kati ya waasi wa M23 na serikali ya Kongo.Picha: Reuters

Rais Yoweri Museveni aliamrisha kufungwa kwa mpaka wa Bunagana Jumanne ya wiki hii kufuatia ombi la rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Joseph Kabila. Kufungwa huku kulithibitishwa na msemaji wa jeshi la Uganda kanali Felix Kulayigye ambaye anasema ilibidi waufunge mpaka huo. Eneo la mpakani la Bunagana ndilo lililokuwa la kwanza kutekwa na waasi wa M23 mwezi wa tano mwaka huu. Hii ni kwa sababu kama eneo la kibiashara lililoko mpakani lina manufaa mengi sana ya kifedha na walihitaji pesa hizo kuendeleza vitendo vyao vya uasi.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.Picha: dapd

Ikikumbukwa kuwa mwezi uliopita shirika la habari la Reuters lilichapisha ripoti ya umoja wa mataifa iliyosema Uganda na Rwanda zinawafathili waasi wa M23, Kinshasa ilitaka mpaka wa Bunagana kufungwa ili watu wanaowafadhili M23 wasipate njia ya kuendelea kuwapa msaada. Ingawa Kanali Kulayigye anasema rais Kabila hakutoa msimamo wake, mwezi uliopita, akizungumza mjini Kinshasa na waandishi habari kutoka Uganda, rais Kabila alisisitiza kuwa

Jeshi la Uganda lashika doria

Jeshi la Uganda limeshika doria pale mpakani ili kuhakikisha kuwa hakuna magari au watu wanaouvuka mpaka wa Bunagana. Tangu mapigano makali kuzuka mwezi wa tano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23, wakongomani wanaoishi karibu na mpaka wa Bunagana wamekuwa wakilala nchini Uganda na asubuhi kurudi kwao kwenda kulima na kuteka maji.

Vifaru vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vikiweka kambi katika mji wa mashariki wa Rumagambo.
Vifaru vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vikiweka kambi katika mji wa mashariki wa Rumagambo.Picha: Reuters

Ahebwa Gideon, naibu kamishna wa wilaya ya Kisoro, wilaya iliyo pale mpakani anasema wakuu wa wilaya hiyo watajadiliana na washika dau mbali mbali nchini Uganda kuona wakongomani walio mpakani Bunagana watasaidiwa vipi. Wafanyibiashara wanaosafirisha bidhaa kama sukari, mafuta ya kupikia, matunda na vyakula vibichi wamekwama pale mpakani pia. Hawajui la kufanya ila kuhesabu gharama wanayoipata.

Mwandishi: Leyla Ndinda
Mhariri: Saum Yusuf Ramadhan