1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda: Mbabazi kutochukua fomu za kugombea urais

Admin.WagnerD16 Julai 2015

Mabishano yaliyozuka kati ya waziri mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya chama tawala NRM Dr. Tanga Odoi yamempelekea kutochukua fomu za kumruhusu kugombea urais wa chama hicho.

https://p.dw.com/p/1G09i
Waziri Mkuu wa zamani wa Uganda Amama MbabaziPicha: Getty Images/AFP/R. Bosch

Huku Mbabazi akitaka mwanzo aoneshwe kanuni na masharti kuhusiana na zoezi hilo kabla ya kulipia fomu za uteuzi, Dr. Odoi amesisitiza kuwa kila mtu atatakiwa kutii utaratibu uliopo na hawezi kumpendelea Mbabazi kwa njia yoyote. Na kama anavyotuarifu mwandishi wetu wa Kampala, Lubega Emmanuel, Mbabazi hakukubaliana na hilo na akaamua kuondoka kwenye makao makuu ya chama hicho.

Mwandishi: Emmanuel Lubega

Mhariri:Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi