UFYATUAJI RISASI VIRGINIA NDIO MADA KUU | Magazetini | DW | 19.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

UFYATUAJI RISASI VIRGINIA NDIO MADA KUU

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya ujerumani umetuwama leo juu ya mada moja kuu:kuuliwa watu 33 katika ufyatuaji risasi shuleni huko Virginia,Marekani.darasa gani ulimwengu umejifunza na vipi haki ya kumliki silaha ?

Likitufungulia pazia gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Lüneburg laandika:

Kwa jinsi Lobi ya wanaotetzea kumiliki silaha nchini Marekani ilivyo na nguvu kubwa,risala ya huzuni inayotokana na mauaji ya Virginia inahakikisha kwamba hata siku za mbele haki hiyo itabakia kwa kila raia kuendelea kumiliki silaha.

Kwani Lobi hiyo ina nguvu kubwa mno.Kwani,jumuiya ya kitaifa ya wanaomiliki bunduki-yenye makao yake huko huko Virginia,inatetea kufa-kupona kuwa haki ya muamerika kumiliki silaha ni nguizo mojawapo ya katiba ya marekani.”

Mod.Hata ikiwa ni hivyo, gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linahadharisha hivi:

Kusema kweli, sheria za kumiliki silaha hasa katika mkoa huu wa Virginia ni laini sana.Wanaotetea haki ya kuweza kufyatua risasi wanapenda sana kuegemeza hoja zao katika katiba na historia ya Marekani.Na wanafanya hivyo kwa mafanikio. Wasio wamarekani wanahisi vigumu kuelewa desturi hiyo inayofuatwa na mamilioni ya waamerika na kupaliliwa na vigogo vya kisiasa.

Na hasa baada ya mkasa wa juzi jumatatu desturi hii inaonekana ni maadili ya kipumbavu.

Gazeti lauliza iwapo mkasa huo wa juzi wa mauaji ungeweza kuepukwa laiti kungekuwapo sharia kali ya kumiliki silaha ?

Kutoa mfano wa Erfurt,kulikozuka mkasa kama huo hapa Ujerumani si sawa,lasema gazeti,kwani Erfurt-gazeti latukumbusha- iko Thüringen na sio Marekani.

Gazeti la NUEE DEUTSCHLAND linalochapishwa mjini Berlin, limegundua kuwa nchini Marekani kuna wendawazimu zaidi wanaofyatua risasi ovyo-ovyo kuliko kwengineko duniani.Laandika:

“Kuwa hata kungelikuwapo sharia kali kusingetosha pekee kuzuwia bahari ya damu,darasa la Erfurt (Ujerumani) na lile la Montreal,Kanada limetufunza.Hatahivyo, hakuna nchi inayokumbwa na mauaji ya halaiki ya watu mashuleni na vyuo vikuu kama Marekani.

Na mabingwa wamegundua chanzo chake nacho ni kuwa hakuna kwengineko ulimwenguni ni rahisi tena kisheria kujipatia bunduki kama Marekani.Hata mstuko uliopata ulimwengu huko Columbine miaka 8 nyuma hautabadili hali hiyo.

Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linalochapishwa Erfurt, laamini kwamba mstuko wa jana hautabadili kitu:

“Dharuba iliovuma ikitulia m kasa uliopita utasahauliwa.Hata huko Virginia hali itarudi kuwa kama zamani.Na hivyo ndivyo ilivyotokea Columbine.Na vivyo hivyo, ilikua Erfurt ….

Umwagaji damu umegeuka biashara nono kuweza kuwashawishi wafanyao biashara hiyo kuachana nayo.Matumizi ya nguvu ni dhahiri kila mahala-katika viwanda vya kuunda silaha.katika studio za filamu na katika maisha ya sasa ulimwenguni.”

Gazeti la MANHEIMER MORGEN linahisi kuwa, si mengi yanayojulikana juu ya chanzo cha bahari ya damu iliomwaika huko Virginia:Limegundua jambo moja wazi-nalo:

“Muuaji ni sehemu ya jamii ambayo inaabudu kumuliki silaha uhuru wa kila mtu na ni alama ya udume.Alifyatua risasi katika mkoa wa Marekani ambamo maseneta au wabunge huvaa bastola wakiingia Bungeni.

Akiishi muaji huyo katika nchi ambako umma husha ngiria pale mchezacinema maarufu Charlton Heston,huku mkono wake ukimtetemeka akinyanyua bunduki yake na akifoka kuwa licha ya uzee wake bado hataweka chini bunduki yake.”

.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com