1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yatarajia wimbi jipya la maambukizi ya corona

Amina Mjahid
30 Juni 2022

Mshauri Mkuu wa kisayansi katika serikali ya Uingereza Jean Francois Delfraissy amesema wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona yaliyosababishwa na aina mpya ya virusi hivyo.

https://p.dw.com/p/4DT6n
Symbolbild Impfung
Picha: Olena Mykhaylova/Zoonar/picture alliance

Mshauri Mkuu wa kisayansi katika serikali ya Uingereza Jean Francois Delfraissy amesema wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona yaliyosababishwa na aina mpya ya virusi hivyo huenda yakashuhudiwa mwishoni mwa mwezi Julai.

Delfraissy amesema wanatarajia pia kirusi aina ya BA 5 kuzuka upya iwapo hakutatokea aina mpya nyengine ya kirusi katika msimu wa mapukutiko.

Ufaransa imeripoti maambukizi mapya 124,724 ya virusi vya corona katika kipindi cha saa 24 zilizopita ikilinganishwa na 77, 967 wiki moja iliyopita.

Wiki hii serikali ya Ufaransa imependekeza raia wake kuanza tena kuvaa barakoa katika maeneo yaliyojaa watu hasa katika usafiri wa umma ili kudhibiti maambukizi zaidi.