Ufaransa yapendekeza Burundi iwekewe vikwazo | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ufaransa yapendekeza Burundi iwekewe vikwazo

Ufaransa imewasilisha mswada wa azimio kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linalopendekeza jumuiya ya kimataifa kuibinya Burundi, huku kukiwa na wasiwasi wa kuweza kutokea mauaji makubwa

UN Sicherheitsrat der Vereinten Nationen

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Hatua hizo zinatishia kuwalenga viongozi wa Burundi wanaochochea machafuko na kuzuia juhudi za kuusuluhisha mzozo uliozuka kufuatia maandamano yaliyotokana na uamuzi wa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu madarakani.

Naibu balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Alexis Lamek amenukuliwa na shirika la habari la ufaransa AFP akisema " Hali ya vurugu nchini Burundi imefikia kiwango cha kuogopesha zaidi,inaweza naweza sema nchani". Balozi aliendelea kusema kwamba lazima wakubaliane na ukweli na kuonya kama wataendelea kuacha mvutano kuendelea kuenea machafuko yataenea nchi nzima.

Nakala ya mswada

Burundi Gewalt in Bujumbura

Operesheni ya kupokonya silaha

Rasimu ya maazimio hayo ambayo, AFP imepata makala yake imetoa wito kwa serikali na pande zote kutokukubaliana na aina yoyote ya vurugu na kulaani vikali mauwaji, mateso, ukamataji watu wa holela na ukiukwaji mwingine wa haki za binaadamu nchini Burundi. Baraza la usalama linataweza kuipigia kura mapendekeo hayo katika siku zijazo.

Katika mkutano huo wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Matiafa lililoitishwa na Ufaransa,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Burundi Alain Aime Nyamitwe amesema hali ni tulivu nchini mwake, isipokuwa katika baadhi ya maeneo yaliyo na shuguli za kile alichosema kumekuwepo na makundi madogo ya wahalifu.

Akuzungumza kwa kutumia mkutano wa moja kwa moja kupitia video akiwa Bujumbura waziri huyo alisema "Burundi haipo haiwaki moto". Na kulitaka baraza la usalama kutotumia vikwazo kwa kusema kwamba havitaleta manufaa yoyote. Aidha alikazia kauli yake kwa kusema serikali inaesendesha mazungumzo na upinzani, kama ilivyohitajiwa na Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Uingereza Matthew Rycroft alitoa wito kwa baraza la usalama kuungana katika kuchukua hatua madhubuti kwa lengo la kudhibiti taifab hilo kutumbika katika kile alichokiita uwezekano wa kutokea mauwaji ya halaiki, kama ilivyotokea Rwanda miaka 21 iliyopita.

Hapo Jumatatu watu wengine wawili waliuawa katika msako mkali wa silaha mjini Bujumbura, siku kadha baada ya vifo vya wengine tisa katika klabu moja ya pombe, vilivyosababisha na mshambuliaji alievalia mavazi ya polisi.

Burundi imegubikwa na vurugu tangu rais Nkurunziza aanzishe jitihada zake tata za kumfanikisha kuongozea muhula wake wa tatu madarakani Aprili, jambo lililosababisha zaidi ya watu 200,000 kulikimbia taifa hilo. Polisi kwa wakati huu wameanzisha operesheni kabambe ya kusaka silaha mikoni mwa watu katika maeneo ya wapinzani katika mji mkuu wa taifa hilo, Bujumbura baada ya siku ya mwisho iliyotelewa na serikali kuzisalimisha silaha hizo kwa hiyari kufikia tamati Jumamosi iliyopita.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com