1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yaomba raia waliofungwa Chad wafungwe nyumbani

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChHF

N’DJAMENA

Ufaransa hapo jana imeitaka Chad kuwarejesha nyumbani wafanyakazi sita wa misaada wa Ufaransa waliohukumiwa vifungo vya miaka minane na kazi ngumu gerezani kwa kujaribu kuwateka nyara watoto 103 wa nchi hiyo.

Wanaume hao wanne na wanawake wawili wa shirika la misaada ya kibindaamu la Ufaransa Zoe Ark walikamatwa hapo mwezi wa Oktoba wakati wakijaribu kuwasafirisha watoto hao wenye umri kati ya mwaka mmoja na kumi kuelekea Barani Ulaya kwa ajili ya kulelewa.

Waziri wa Sheria wa Ufransa Rachida Dati ameomba rasmi kwa watu hao kuhamishiwa Ufaransa kutumikia vifungo vyao chini ya makubaliano ya kisheria ya mwaka 1976 kati ya Ufaransa na koloni lake hilo la zamani.