1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa wapania kutinga robo fainali

28 Juni 2021

Ufaransa watakuwa wanapambana na Uswisi. Ufaransa waliebuka washindi wa kundi gumu F baada ya kutoa ushindi katika mechi moja na kutoka sare mbili.

https://p.dw.com/p/3vh8l
UEFA Nations League | Portugal vs. Frankreich | Jubel Frankreich
Picha: Rafael Marchante/REUTERS

Kocha wao Didier Deschamps ana kibarua kigumu kwani baadhi ya wachezaji wake nyota hasa katika safu ya ulinzi wamepata majeraha.

Jules Kounde na Lucas Digne ndio wachezaji ambao wataikosa mechi hii ya leo ila Lucas Hernandez huenda akashirikishwa baada ya kuonesha matumaini kutokana na jeraha la goti alilopata.

"Unapocheza mechi ya kwanza ya makundi unajua bado kuna mechi mbili zaidi ila sasa tutacheza na nia ya kufika robo fainali. Hili litafanyika tu iwapo tutawafunga Uswisi. Katika raundi ya kwanza Italia walicheza vizuri mno ila ungwe ya mtoani dhidi ya Austria, haikuwa rahisi, walipata ushindi kwa tabu sana. Unastahili kujiandaa vyema, kawaida kuna wachezaji wazuri katika timu pinzani na ndivyo itakavyokuwa leo," alisema Didier Deschamps.

Mlinda lango wa Ufaransa ambaye pia ni nahodha Hugo Lloris yeye ana matumaini makubwa na Les Bleus kuelekea mpambano wa leo.

EURO 2021 |  Türkei vs Schweiz | Jubel
Wachezaji wa Uswisi wakisherehekea goli walilofunga dhidi ya UturukiPicha: Darko Vojinovic/AP Photo/picture alliance

"Tunaanza mashindano mapya sasa , jinsi tutakavyojiandaa kuicheza mechi hii ni tofauti, tunajua hatustahili kufanya makosa. Tuna timu yenye washambuliaji wazuri sana na wamefanya vyema miaka iliyopita . Tunajua ni mechi ambayo tunastahili kujiandaa vyema kisaikolojia ili tuishinde ila tunastahili kuonyesha mchezo wa hali ya juu ili tufuzu raundi inayofuata," alisema Lloris.