UEFA Champions League kurejea uwanjani | Michezo | DW | 05.11.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

UEFA Champions League kurejea uwanjani

Ligi ya mabingwa barani Ulaya ,Champions League ,Barca, Manchester United na Porto huenda zikakata tikiti zao kuingia katika michuano ya awamu ya mtoano wiki hii (06.11.2012)

Real Madrid's Goalkeeper Iker Casillas (L-R) saves the ball in front of Dortmunds Mats Hummels and Robert Lewandowski during the Champions League Group D soccer match between Borussia Dortmund and Real Madrid at BVB Stadium Dortmund in Dortmund, Germany, 24 October 2012. Photo: Kevin Kurek/dpa

Borussia Dortmund -ilipopambana na Real Madrid katika Champions League

Bayern Munich yazidi kupaa bila mpinzani ligi ya Ujerumani Bundesliga, mabingwa watetezi Borussia Dortmund bado yasua sua.na huko nchini Kenya timu tatu zawania ubingwa wa ligi ya nchi hiyo ikiwa umesalia mchezo mmoja tu hapo Jumamosi(10.11.2012)

Bayern Munich imeonesha msimu huu kuwa haina mpinzani, baada ya kupata ushindi wake wa tisa mwishoni mwa Juma baada ya kuizaba Hamburg SV kwa mabao 3-0. Baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Bayer Leversen wiki iliyopita, Bayern imejitutumua na kuongeza kasi katika msimamo wa ligi ambapo inaongoza sasa kwa points saba ikiiacha nyuma timu inayoifuatia Schalke 04 , ambayo ina points 20.

Bayern's players celebrate after scoring during the German Soccer Cup match (DFB Pokal) between FC Bayern Munich and 1. FC Kaiserslautern in Munich,Germany Wednesday, Oct. 31, 2012. (Foto:Kerstin Joensson/AP/dapd)

Bayern München yazidi kutisha Bundesliga

Einchracht Frankfurk inafuatia ikiwa nayo na points 20 na Bayer Leverkusen imeipiku Borussia Dortmund katika nafasi ya nne ikiwa na points 18 wakati mabingwa hao watetezi Borussia wako katika nafasi ya tano sasa wakiwa na points 16.

Michezo ya Jumapili (05.11.2012) ya kufunga mchezo huo wa 10 wa Bundesliga ilizikutanisha timu za Werder Bremen na Mainz 05 , na Bayer Leverkusen ilikuwa ikionyeshana kazi na Fortuna Dusseldorf. Werder Bremen ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mainz 05 na Leverkusen ikatwaa points zote tatu dhidi ya Fortuna Dusselsdorf kwa ushindi wa mabao 3-2.

Mabingwa watetezi Borussia Dortmund walitoka sare bila kufungana na VFB Stuttgart siku ya Jumamosi na kwa mabingwa hao sare ni sawa na kushindwa.

Fußball Bundesliga, 10. Spieltag, Borussia Dortmund - VfB Stuttgart am 03.11.2012 im Signal Iduna Park in Dortmund. Dortmunds Sebastian Kehl (am Boden) liegt nach einem Zusammenprall mit Stuttgarts Raphael Holzhauser (r) verletzt am Boden. Foto: Bernd Thissen/dpa (Achtung Sperrfrist! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung der Bilder im IPTV, Mobilfunk und durch sonstige neue Technologien erst zwei Stunden nach Spielende. Die Publikation und Weiterver­wertung im Internet ist während des Spiels auf insgesamt fünfzehn Bilder pro Spiel begrenzt. ) +++(c) dpa - Bildfunk+++

Nahodha wa Borussia Dortmund Kiel akiwa amejeruhiwa

Champions League.

Barcelona, Manchester United , FC Porto na pengine Malaga huenda wakakata tikiti zao kuelekea awamu ya mtoano katika Champions league wiki hii ikiwa timu hizo zitashinda michezo yake. Timu hizo nne zimekwisha shinda michezo yao yote mitatu ya mwanzo katika makundi yao na iwapao timu hizo zitashinda mchezo wa nne zitakuwa tayari zimekata tikiti zao tayari kwa michuano ya mtoano.

Schalke 04 , Borussia Dortmund na Shakhtar Donetsk huenda nazo zikajiweka katika mazingira mazuri ya kuingia katika michuano ya mtoano ikiwa zitapata ushindi , wakati mabingwa watetezi Chelsea , Manchester City na mabingwa wa zamani Juventus Turin ziko katika hali ngumu kidogo.

Champions League inafikia katika wakati muhimu sana na hatuwezi kuruhusu makosa mengine yoyote, amesema kocha wa Arsenal London , Arsene Wenger.

Arsenal's manager Arsene Wenger reacts as he watches his team play against Queens Park Rangers during their English Premier League soccer match at Emirates Stadium, London, Saturday, Dec. 31, 2011. (AP Photo/Sang Tan)

Arsene Wenger, kocha wa Arsenal London

Baada ya ushindi dhidi ya Montpellier na Olympiakos Piraeus katika michezo yao miwili ya awali katika kundi B, Arsenal iliteleza na kuangukia miguuni pa Schalke kwa kufungwa mabao 2-0 nyumbani wiki mbili zilizopita na ikishindwa tena katika ardhi ya Ujerumani matumaini ya timu hiyo yatakuwa yamewekwa katika mizani.

Chelsea yasua sua

Chelsea ambayo ilikuwa na mwanzo wa kawaida wa utetezi wa taji lao kwa ushindi, sare na kufungwa, hawawezi tena kuhimili kipigo kingine nyumbani kwa Shakhtar Donetsk, baada ya kupata kipigo nchini Ukraine wiki mbili zilizopita.

Real Madrid inatafuta kulipiza kisasi kwa haraka dhidi ya Borussia Dortmund hapo kesho baada ya kupata kipigo bila kutarajia cha mabao 2-1 wiki mbili zilizopita nchini Ujerumani.

Ushindi wa Borussia Dortmund una maana kuwa timu hiyo inaongoza kundi la D ikiwa na points 7, moja zaidi ya Real , Ajax ikiwa na points 3 na Manchester City wakiwa na piint moja tu.

Utajiri wa Manchester City hautakuwa na maana iwapo timu hiyo itashindwa kutamba mbele ya Ajax Amsterdam kesho Jumanne katika uwanja wa Etihad.

Wakati huo huo wataalamu wa utabibu wanatengeneza kifaa cha kulinda uso ambacho kitamruhusu nahodha wa Borussia Sebastian Kiel kucheza katika mchezo kati ya timu yake na Real Madrid. Kiel alivunjika pua katika mchezo wa Bundesliga ambapo Borussia ilitoka sare ya bila kufungana na VFB Stuttgart, siku ya Jumamosi.

Kikosi cha Jose Mourinho kilijipasha moto kwa mchezo wa kesho kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Real Zaragoza katika La Liga nchini Uhispania lakini hawakuwa katika hali yao nzuri licha ya kiwango hicho cha mabao.

Real Madrid's coach Jose Mourinho from Portugal reacts during a semi final second leg Champions League soccer match against Bayern Munich at the Santiago Bernabeu stadium, in Madrid, Wednesday, April 25, 2012. (Foto:Daniel Ochoa de Olza/AP/dapd)

Jose Mourinho wa Real Madrid

Kukosekana kwa Xabi Alonzo na Sami Khedira ambaye ni majeruhi , Mourinho aliteremsha uwanjani kikosi chenye baadhi ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu kama Michael Essien na Luka Modric katika sehemu ya kati lakini hawakuwa na udhibiti unaohitajika.

Hata hivyo Alonzo atarejea kundini dhidi ya Borussia , lakini Khedira ana shaka kuanza mchezo huo.

Pique kunduni

Wakati huo huo mlinzi wa kati wa Barcelona Gerard Pique amerejea kundini baada ya kuwa majeruhi na sasa yuko fit kukabiliana na Celtic katika mchezo wa kundi G katika champions League.

Mchezaji bora wa Afrika

Na katika bara la Afrika mshindi wa mwaka jana wa taji la mchezaji bora wa Afrika Yaya Toure anaongoza orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo, ambayo itatangazwa rasmi mwezi ujao, limesema shirikisho la kandanda barani Afrika CAF.

Toure anajiunga na wachezaji wengine wa Cote I'Ivoire , Didier Drogba na Gervinho katika orodha hiyo ya watu kumi. Mshambuliaji wa Newcastle United Demba Ba, John Obi Mikel wa Chelsea na mchezaji wa zamani wa kiungo wa Arsenal Alexandre Song wanapatikana katika orodha hiyo ambayo inawakilisha wachezaji wanaosakata kandanda nchini Uingereza katika premier League. Pia wamo Younes Belhanda wa Morocco , na Chris Katongo wa Zambia.

Fußball Freundschaftsländerspiel: Deutschland - Elfenbeinküste am Mittwoch (18.11.2009) in der Veltins-Arena in Gelsenkirchen. Yaya Toure von der Elfenbeinküste gedenkt des verstorbenen deutschen Nationaltorhüters Enke. Foto: Rolf Vennenbernd dpa/lnw

Yaya Toure mchezaji bora wa mwaka wa Afrika 2011.

Wakati huo huo , ligi ya soka nchini Kenya inafikia ukingoni Jumamosi hii(10.11.2012) , ambapo vigogo wa zamani wa soka la Kenya Gor Mahia na AFC Leopards , wanakaribia kabisa kutawazwa mabingwa wa ligi hiyo. Gor Mahia ambayo inakaribia kunyakua ubingwa wake wa kwanza kabisa wa Premier League baada ya miaka 15 iliikandika Muhoroni Youth kwa mabao 4-0 Jumapili(05.11.2012) katika uwanja wa jiji la Nairobi, Nairobi City Stadium.

Na huko nchini Msumbiji Maxaquene FC ndio iliyotawazwa mabingwa wa ligi daraja la kwanza nchini humo mwishoni mwa juma baada ya ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Textil Pungue jana Jumapili(05.11.2012).

Baada ya sare waliyoipata mahasimu wao Ferroviario Maputo , ina maana Maxaquene inaongoza kwa points sita ikiwa bado michezo miwili. Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Maxaquene tangu mwaka 2003 na wa tano kwa jumla tangu pale Msumbiji ilipojipatia uhuru kutoka Ureno mwaka 1975.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe /dpae

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman