Udhalilishaji kingono umeenea Congo | Matukio ya Afrika | DW | 19.06.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Udhalilishaji kingono umeenea Congo

Maelfu  ya  wasichana  wadogo  wamekamatwa  ama kuingizwa  katika  majeshi  ya  wanamgambo kadhaa mashariki  mwa  Jamhuri  ya  kidemokrasi  ya  Congo.

Maelfu  ya  wasichana  wadogo  wamekamatwa  ama kuingizwa  katika  majeshi  ya  wanamgambo kadhaa mashariki  mwa  Jamhuri  ya  kidemokrasi  ya  Congo, ambako  mara nyingi  wanatumika  kingono , kundi  la kutetea  haki  za  watoto  la  Child Soldiers International limesema  leo.

Mashariki  mwa  Congo  kuna  mamia  kwa  maelfu  ya wanajeshi  watoto  na  wasichana  ambao  wanahusiana na  makundi  hayo  yenye  silaha, amesema  Sandra Olsson kutoka  kundi  hilo  la  Child Soldiers International.

Wasichana  wenye  umri kutoka  miaka  tisa  hadi  16 wanafanya  kazi   mbali  mbali  kwa  ajili  ya  wanamgambo, ikiwa  ni  pamoja  na  kupika, ukusanya  kuni, kubeba  mali zilizoporwa, wakitumika  pia  kama  watumwa  wa  kingono na  hata  kushiriki  katika  mapigano  kama  wanajeshi  ama wapelelezi, Olsson  ameliambia  shirika  la  habari  la  dpa.

Kundi  la  Child Soldiers International  pamoja  na washirika  wake  wa  Congo wamewahoji wasichana  150 kwa  ajili  ya  ripoti  itakayochapishwa  leo.