Uchumi wa Ujerumani wakua zaidi. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 14.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Uchumi wa Ujerumani wakua zaidi.

Uchumi wa Ujerumani umekuwa zaidi katika eneo la nchi zinazotumia sarafu ya Euro katika robo ya pili ya mwaka 2010.

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Rainer Bruederle.

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Rainer Bruederle.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu mjini Wiesbaden, pato la ndani la Ujerumani limeongezeka kwa asilimia 2.2 ukilinganisha na robo ya kwanza ya mwaka huu.

Hali hiyo imefanya kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa tokea kuunganika tena kwa Ujerumani miaka 20 iliyopita.

Commerzbank AG Deutschland Frankfurt

Moja ya benki nchini Ujerumani zilizonufaika na kukua kwa uchumi wa nchi.

Mkuu wa kitengo cha uchumi katika kampuni ya uwekezaji ya DekaBank, Holger Bahr amesema ukuaji huo umetokana sana na usafirishaji wa bidhaa nje na uwekezaji.

Aidha Pato la ndani la Ufaransa pia limeongezeka kwa asilimia 0.6 kwa kipindi cha miezi minne iliyopita, huku Uhispania uchumi wake ukiongezeka kwa asilimia 0.2.

 • Tarehe 14.08.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OnXe
 • Tarehe 14.08.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OnXe
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com