Uchaguzi wafanyika Pakistan. | NRS-Import | DW | 18.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Uchaguzi wafanyika Pakistan.

ISLAMABAD.

Wananchi milioni 80 wa Pakistan wametolewa mwito wa kupiga kura leo kulichagua bunge jipya ,ambapo kwa mujibu wa kura za maoni, chama cha upinzani cha Pakistan People's Party kinatarajiwa kushinda.Hadi mwezi desemba chama hicho kilikuwa kinaongozwa na hayati Benazir Bhutto alieuliwa katika shambulio la kigaidi.

Uchaguzi wa leo unatathminiwa kama kura ya maoni itakayoamua mustakabali wa rais Pervez Musharraf.Kiti cha rais huyo kinaweza kuyumba ikiwa vyamavya upinzani vitashinda katika uchaguzi wa leo.

Chama kingine cha upinzani kinachotarajiwa kushika nafasi ya pili ni cha Muslim League cha bwana Nawaz Sharif aliewahi kuwa waziri mku

wa Pakistan.

Watu wataanza kupiga kura saa mbili asubuhi.

kutokana na wasiwasi mkubwa wa kutokea mashambulio ya kigaidi,wanajeshi alfu 80 watasaidiana na polisi katika kulinda usalama. Matokeo ya kwanza yanatarajiwa kufahamia leo usiku.

 • Tarehe 18.02.2008
 • Mwandishi Abdu Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8zi
 • Tarehe 18.02.2008
 • Mwandishi Abdu Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8zi
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com