1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa urais waaihirishwa tena Lebanone

29 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Chgp

BEIRUT

Uchaguzi wa Rais nchini Lebanon uliokuwa umepangwa kufanyika leo hii umeahairishwa kwa mara nyengine tena.

Spika wa bunge la Lebanone Nabih Berri amesema katika taarifa kwamba uchaguzi huo utafanyika wakati wa kikao kijacho cha bunge hapo tarehe 12 mwezi wa Januari.Hii ni mara ya 11 kwa uchaguzi huo kuahirishwa ambao awali ulikuwa ufanyike miezi mitatu iliopita kwenye bunge na hiyo kuufanya mgogoro wa kisiasa nchini humo uzidi kupamba moto na mbaya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo tokea kuzuka kwa vita vya wenyewer kwa wenyewe vya mwaka 1975 hadi mwaka 1990.

Wadhifa huo umekuwa wazi tokea Emil Lahoud anayeungwa mkono na Syria kumalizika muda wake hapo tarehe 23 mwezi wa Novemba.

Serikali tawala ya mseto inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na upinzani unaongozwa na kundi la Hezbollah wamekubaliana juu ya Mkuu wa majeshi Generali Michael Suleiman kushika wadhifa huo wa urais lakini bado wanajadili juu ya namna ya kushirikiana maadaraka katika serikali mpya itakayoundwa mara tu baada ya rais huyo kuingia madarakani.