1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa urais Libya wakumbwa na wasiwasi

John Juma
15 Desemba 2021

Uchaguzi wa rais nchini Libya unaokusudiwa kuiunganisha nchi, unatarajiwa kufanyika ndani ya wiki moja kutoka sasa, lakini miito ya kutaka uchaguzi huo uahirishwe ni mingi.

https://p.dw.com/p/44HpB
Saif al-Islam al-Gaddafi, son of Libya's former leader Muammar al-Gaddafi, registers as a presidential candidate in Sebha
Picha: Khaled Al-Zaidy/Handout/Reuters

Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa kiungo cha kuiunganisha nchi iliyogawika baada ya muongo mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Lakini bado kuna mashaka.

Uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Disemba 24, utakuwa wa kwanza wa urais tangu kuuawa kwa Muammar Gaddafi, dikteta aliyeitawala nchi hiyo kwa Zaidi ya muongo mmoja.UN yafuatilia majaribio ya kuzuia mchakato wa uchaguzi Libya

Kwa muda wa karibu mwaka mmoja sasa, uchaguzi huo umekuwa lengo kuu la juhudi za kimataifa kuleta amani katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta kaskazini mwa Afrika. Wanaounga mkono uchaguzi wanahofia hali ya hatari ikiwa hautafanyika kama ulivyopangwa.

Tahadhari ya wakosoaji

Lakini wakosoaji wanatahadharisha kwamba kuendelea na mipango ya uchaguzi kunaweza kuitumbukiza nchi katika machafuko mapya. Wanasema Libya ingali imegawika zaidi baina ya pande zenye silaha. Na kuna uwezekano kwamba zitayapinga matokeo ikiwa ushindi utaenda kwa wapinzani wao.

Takriban watu 100 wametangaza kuwania urais. Tume inayosimamia uchaguzi ilitarajiwa kutangaza orodha rasmi ya wagombea wiki iliyopita, lakini haijatoa orodha orodha hiyo rasmi kwa sababu ya mapingamizi ya kisheria.

Utata kuhusu sheria ya uchaguzi

Libya ilitumbukia kwenye machafuko baada ya kifo cha Moammar Gaddafi mwaka 2011 kufuatia maandamano makubwa yaliyoungwa mkono na kampeni ya kijeshi kutoka Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Kwa miaka mingi nchi hiyo imegawika kati ya pande pinzani za kiutawala kutoka mashariki na magharibi, kila upande ukiwa unaungwa mkono na wanamgambo pamoja na serikali za kigeni.

Uwepo wa baadhi ya watu wenye ushawishi lakini ambao pia wamechangia pakubwa mgawanyiko wa Libya, katika kinyang'anyiro cha urais akiwemo mwanaye rais wa zamani Moammar Gaddafi- Seif al-Islam unafanya hali kuwa hata tete zaidi.
Uwepo wa baadhi ya watu wenye ushawishi lakini ambao pia wamechangia pakubwa mgawanyiko wa Libya, katika kinyang'anyiro cha urais akiwemo mwanaye rais wa zamani Moammar Gaddafi- Seif al-Islam unafanya hali kuwa hata tete zaidi.Picha: Ayhan Mehmet/AA/picture alliance

Mchakato wa sasa wa kisiasa ulianza mwaka uliopita baada ya mapigano mabaya ya mwisho.

Utata kutokana na baadhi ya wagombea urais

Mtoto wa Ghaddafi, Seif Al Islam kuwania urais wa Libya

Mnamo Aprili 2019, kamanda wa kijeshi ambaye vikosi vyake vinadhibiti mashariki mwa Libya Halifa Haftar alianzisha mashambulizi yaliyolenga kuukamata mji mkuu Tripoli, na kuangusha serikali inayotamb uliwa na Umoja wa Mataifa iliyoko katika mji huo.

Haftar alikuwa akiungwa mkono na Urusi, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu. Uturuki na Qatar ziliongeza juhudi zao za kuunga mkono wanajeshi wa serikali iliyoko Tripoli kwa kuwapa silahaza za hali ya juu, wanajeshi pamoja na mamluki kutoka Syria.

Baada ya miezi 14 ya mapigano, upande wa Haftar ulilemewa. Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoongozwa na Umoja wa Mataifa yakafikiwa Oktoba 2020. Kisha kundi lijulikanalo kama Jukwaa la Kisiasa la Libya likaandaa dira au muongoza wa kuundwa kwa serikali ya mpito kuiongoza nchi hadi uchaguzi utakapofanyika Disemba 24.

Wale wanaotaka uchaguzi uahirishwe wanahoji kuna hali ya juu ya kutoaminiana kati ya viongozi wa upande wa mashariki na magharibi. Hali inayofanya mambo kuwa tete zaidi.

Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesema, serikali ya mpito nchini Libya haijafaulu kuunganisha taasisi za nchi hiyo hususan jeshi, wala kuvunja makundi ya wanamgambo au hata kuhakikisha mamluki pamoja na wapiganaji wa kigeni walioko wanaondoka.

Kujikokota kwa juhudi za kusuluhisha masuala tete

”Masuala haya yalipaswa kuwa yameshasuluhishwa kabla ya uchaguzi. Wanahitaji muda na juhudi zaidi kuyatatua,” amesema afisa wa Umoja wa Mataifa ambaye hakutaka kutambulishwa jina kwa kuwa haruhusiwi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Tarek Mitri ambaye ni mjumbe wa zamani wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ametahadharisha kuwa ”bila ya pande pinzani za kijeshi kuunganishwa, uchguzi huo utakuwa kama kitisho dhidi ya amani.”

”Ni vipi unaweza kushinda uchaguzi wa kidemokrasia unaoandaliwa katika mazingira ambayo pande pinzani zimejihami vilivyo kwa bunduki zilizojazwa risasi?” Mitri ameuliza swali hilo huku akielezea mashaka yake na uchaguzi huo.

Sheria kuhusu uchaguzi pia inakosolewa, huku wanasiasa kutoka magharibi mwa Libya wakilituhumu bunge lililoko mashariki mwa nchi hiyo kwa kuidhinisha sheria hizo bila ya kuwashirikisha.
Sheria kuhusu uchaguzi pia inakosolewa, huku wanasiasa kutoka magharibi mwa Libya wakilituhumu bunge lililoko mashariki mwa nchi hiyo kwa kuidhinisha sheria hizo bila ya kuwashirikisha.Picha: Hamza Alahmar/AA/picture alliance

Katika juhudi za mwisho kuunusuru uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alimteua mwanadiplomasia wa Marekani Stephanie Williams aliyeyaongoza mazungumzo ya kusitisha vita Oktoba 2020, kama mshauri wake maalum kuhusu masuala ya Libya.

Williams alikutana na maafisa wa Libya mjini Tripoli siku ya Jumapili.

Himizo kwa pande zoze kuheshimu matakwa ya wananchi

Alizitaka pande zote kuheshimu haja kubwa ya wananchi kuwachagua viongozi wao kwa njia huru, wazi na kwenye uchaguzi wa kuaminika. Hata hivyo katika hotuba yake hadharani hakutaja tarehe ya uchaguzi Disemba 24.

Marekani na washirika wengine wa kimataifa wanataka uchaguzi huo kuendelea mbele kama ulivyopangwa. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeondoka Libya Disemba 8, Jan Kubis alisema uchaguzi huo ni sharti ufanyike kulingana na ratiba akisema ni kitu muhimu sana kitakachofungua milango ya masuluhisho ya siku zijazo.

Utata kuhusu uchaguzi huo ulitanda zaidi baada ya Haftar na Seif al-Islam walipotangaza kujitosa kwenye kinyang’anyiro.

Haftar anayetizamwa kama shujaa upoande wa mashariki anachukiwa na wengi upande wa magharibi mwa nchi.

Aidha wengine pia wanatizama hatua ya Seif al-Islam kuwania kama uwezekano wa Libya kurejea katika enzi za udikteta.

(AFPE)