Uchaguzi wa Serbia | Magazetini | DW | 23.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Uchaguzi wa Serbia

Uchambuzi ulituwama juu ya uchaguzi wa Serbia na pendekezo la kuwaacha huru magaidi wa zamani wa jeshi la RFA.

Gazeti la BERLINER ZEITUNG laandika:

„Jeshi la RAF haliko tena.Ukurasa huo wa historia ya Ujerumani ulioandikwa kwa damu haukusahaulika ,lakini kisa chake kimepita.Ikiwa sasa serikali itaamua Bibi Brigitte Mohnhaupt na mwenzake Christian Klar kuwapa msamaha ,msamaha huo , hauwafikii magaidi hao wa zamani bali walionusurika na maisha.Ni sawa kwahivyo, kuwasamehe kwani ,nchini Ujerumani,hakuna adhabu ya kifo ya kuwapitishia.“

Ama gazeti la STUTTGARTER ZEITUNG linasema kuwa, mshtaki mkuu wa serikali ambae mara moja aliwahi kuwa shabaha ya hujuma za jeshi la RAF na angefaa kuwa na hisia juu ya swali hili, amependekeza kuachwa huru kwa Bibi Mohnhaupt…Ujerumani imerejea katika hali ya utulivu na ya kawaida.Na hii, haikutokea hivi hivi tu.“tunaweza kujivunia kidogo yaliotendeka kuleta hali hii“

Gazeti la MANNHEIMER MORGEN linahisi ni vyema kwa dola kama lilivbyofanya siku za nyuma kunyosha mkono wa suluhu bila lakini, kutotia maanani uchungu wa wahanga.Kwani, intafahamika kuona kizuka wa marehemu Hanns-Martin Schelyers akipinga kuachwa huru huko kwa magaidi hao wa zamani.Juu ya hivyo kuchukua hatua kama hiyo ni kutoonesha udhaifu wa dola bali nguvu za jamii hii.

Gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG linasema kuna wengine watakuwa na maoni mengine juu ya kuachwa huru kwa magaidi hao wa zamani.hatahivyo, lasema gazeti-kuwaacha huru hakutatia ila dola hili la kisheria ikiwa litawapa wahalifu hao wakubwa nafasi ya pili.Hii itaonesha wema wa dola.

Likitugeuzia mada, gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linauchambua uchaguzi wa jumapili iliopita nchini Serbia-zamani sehemu ya Yugoslavia.Uchaguzi huo haukutoa sura wazi na hivyo gazeti laandika:

„Wazi ni kuwa haipendezi kuona chama cha Socialist Party cha Vojislaw Seseljs na wazalendo wenye siasa kali walionyuma ya Slobodan Milosevic kimejipatia thuluthi-moja ya kura.

Hatahivyo, hayo ni matokeo ya uchaguzi wa kidemokrasi uliopita bila ya fujo lolote.Miaka michache tu nyuma hali kama hiyo haingewezekana… Mtihani hasa kwa demokrasia nchini Serbia utakuja pale uhuru wa jimbo la Kosovo utakapotangazwa- ni maoni ya Frankfurter Allgemeine.

Ama gazeti la KÖLNISCHE RUNDSCHAU linaona kuwa vyama vya kidemokrasi nchini Serbia ingawa vimeshinda uchaguzi, bado havijakamilisha ushindi.Kujipatia ushindi kamili, kunahitajika muwafaka kati ya vyama vilivyohasimiana kwa miaka mingi .Hasa waziri mkuu Kostunica anabidi kukiuka kivuli chake na kumuachia wadhifa wake mshirika wa chanda na pete wa rais Boris Tadic.

Gazeti la NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld linaona cheche za moto ziko katika swali la Kosovo:

Linasema kwamba, mkoa wa Kosovo kimila na utamduni ni shina la waserbia ni jambo moja. Kwamba mkoa huo unakaliwa na wakaazi wengi mno wa ki-albania na wapewe uhuru wao, ni swali jengine.Ukweli huu mchungu hakuna hata chama kimoja cha kidemokrasia nchini Serbia kilichothubutu kuudhukuru.Bila ya suluhisho juu ya Kosovo,mlango kuingia Serbia Ulaya utabaki umekomewa na bila UU Serbia haina mustakbala mwema…