Uchaguzi wa rais nchini Zambia. | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.10.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Uchaguzi wa rais nchini Zambia.

Watu wa Zambia leo wanapiga kura kumchagua rais atakaechukua nafasi ya hayati Levy Mwanawasa aliefariki mnamo mwezi agosti.

Nani ataweza kushughulikia mustakabal wa watoto hao baada ya uchaguzi wa leo nchini Zambia?

Nani ataweza kushughulikia mustakabal wa watoto hao baada ya uchaguzi wa leo nchini Zambia?

Watu wa Zambia leo wanapiga kura kumchagua rais atakaechukua nafasi ya hayati Levy Mwanawasa aliefariki mwezi agosti kutokana na kiarusi.

Kinyang'anyiro cha leo ni baina ya kaimu rais, Rupiah Banda na kiongozi wa chama cha upinzani Michael Sata.

Watu wanaendelea kupiga kura na habari zinasema zoezi hilo linafanyika huku kukiwa na mvutano. Vituo kadhaa vilifunguliwa kwa kuchelewa mjini Lusaka. Kiongozi wa upinzani bwana Sata amedai kuwapo njama baina ya maafisa wa tume ya uchaguzi na polisi.

Habari zinasema bwana Sata yupo sambamba na kaimu rais Banda katika kinyang'nyiro hicho. Bwana Sata amesema kuwa chama kinachotawala hakiwezi kushinda katika uchaguzi wa leo .Amedai kuwa tume ya uchaguzi na polisi wanakula njama za kujaribu kuiba kura.

Rais wa muda bwana Rupiah Banda ameahidi kuendelea na sera za hayati Mwanawasa aliekuwa maaruf miongoni mwa watu wake.

Bwana Banda mwenye umri wa miaka 71 anakiongoza chama kinachotawala -Movement For Multi Party Democracy.

Mshindani wake, kiongozi wa chama cha upinzani- Patriotic Front bwana Michael Sata ameahidi kuleta mabadiliko makubwa mnamo muda wa siku 90 . Amesema ikiwa atashinda katika uchaguzi, baada ya muda huo atayalazimisha makampuni ya nje kutoa asilimia 25 ya maslahi yao kwa kampuni za wanananchi wa Zambia.

Licha ya kuwapo mvutano, watazamaji wa kimataifa kutoka Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi unaenda vizuri na kwamba hakuna dalili za kuthibitisha wizi wa kura.


Hatahivyo kutokana na kuhofia kutokea fujo baada ya kumalizika zoezi la kipiga kura leo jioni ,polisi na wanajeshi wamewekwa katika hali ya tahadhari.

Wagombea wengine katika uchaguzi wa leo ni kiongozi wa chama cha UPND bwana Hakainde Hichilema na aliekuwa makamu wa rais, Godfrey Miyanda wa chama cha Heritage. Matokeo ya kwanza yanatarajiwa kufahamika baadae leo.
 • Tarehe 30.10.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FkLM
 • Tarehe 30.10.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FkLM
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com