Uchaguzi wa rais Montenegro | Habari za Ulimwengu | DW | 06.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Uchaguzi wa rais Montenegro


PODGORICA:

Wapiga kura wa Montenegro wanateremka vituoni hii leo kumchagua rais mpya.Uchaguzi huo unaangaliwa kama fursa ya kupima umaarufu wa chama cha wasoshiliasti wa kidemokrasi-DPS kinachotawala nchini humo tangu miongo miwili iliyopita.Utafiti wa hivi karibuni wa maoni ya wananchi umeonyesha rais anaemaliza wadhifa wake Filip VUJANOVIC,mshirika wa waziri mkuu anaependwa na wananchi Milo DJUKANOVIC ana nafasi nzuri ya kunyakua asili mia 50 ya kura na kuepukana na kishindo cha duru ya pili ya uchaguzi.Wapiga kura katika jamhuri hiyo ya zamani ya Yugoslavia,walipiga kura miaka miwili iliyopita kujitenga na jirani yao mwenye nguvu- jamhuri ya Serbia.Mgombea mashuhuri wa upande wa upinzani NEBOJSA MEDOJEVIC anakilaumu chama tawala cha DPS kuhuzsika na rushwa.Mgombea mwengine ANDRIJA MANDIC amefanya kampeni ya kuimarisha mafungamano ya Montenegro na serikali za mijini Belgrade na Moscow.Jamhuri hiyo ya Montenegro yenye wakaazi laki sita na nusu inajivunia ukuaji wa kliuchumi na kutegemea kujiunga haraka na Umoja wa ulaya.

 • Tarehe 06.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dcsu
 • Tarehe 06.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dcsu
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com