1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa rais Georgia

5 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Ckev

TIBILISI:

Uchaguzi wa urais umeanza nchini Georgia.Rais Mikhail Saakashvili ameitisha uchaguzi huu na mapema baada ya polisi wa kuzuwia fujo kupambana vikali na wapinzani wa serikali yake mjini Tibilisi, mji mkuu wa Georgia Novemba mwaka jana.Rais Saakashvili alilaumiwa sana kwa kukandamiza kwa mabavu maandamano hayo ya amani.

Rais Saakashvili ni miongoni mwa watetezi 7 katika uchaguzi wa leo na wachunguzi wanatumai atachaguliwa tena.