Uchaguzi wa kihistoria wafanywa Sudan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 11.04.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Uchaguzi wa kihistoria wafanywa Sudan

Uchaguzi wa kihistoria wa vyama vingi unafanywa nchini Sudan, baada ya zaidi ya miongo miwili.

Symbolbild politische Spaltung im Sudan vor der Präsidentschaftswahl. Karte Sudan mit Hauptstadt Khartoum und Darfur und Südsudan. Vorne: Präsident Al Bashir. 2010_04_01_symbolbild_sudan_spaltung.psd

Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan.

Chaguzi za rais,bunge na serikali za mitaa zinafanywa kuanzia leo tarehe 11 hadi 13 Aprili, licha ya kususiwa na vyama vingi vikuu vya upinzani. Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir anatazamiwa kushinda, baada ya wagombea wawili wakuu kujitoa katika kinyanganyiro hicho.

Yasser Arman, Presidential candidate of Sudan Peoples' Liberation Movement (SPLM), waves to his supporters in Khartoum, Sudan, Thursday, Jan 21,2010. (AP Photo/Abd Raouf)

Kiongozi wa chama cha SPLM, Yasser Arman.

Yasser Arman wa chama cha SPLM kutoka Sudan ya Kusini na Sadiq al Mahdi wa chama cha Umma kutoka kaskazini ya nchi, walitazamiwa kutoa changamoto kali katika uchaguzi wa kugombea wadhifa wa rais. Lakini vyama vingi vya upinzani vimekataa kushiriki katika uchaguzi huo kwa madai kuwa kulikuwepo ila katika utaratibu wa maandalizi ya uchaguzi.

Baadhi ya waangalizi wana wasiwasi kuwa uchaguzi huo na hasa matokeo ya kwanza ya uchaguzi huenda yakazusha machafuko katika nchi iliyoteketezwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwenye hatari kubwa zaidi kwa machafuko kuibuka ni jimbo la Darfur ambako Umoja wa Mataifa unatathmini kuwa kama watu 300,000 wameuawa tangu mapigano yalipoanza katika jimbo hilo la magharibi hapo mwaka 2003.

Mwandishi: Martin,Prema/RTRE

Mhariri: Nyanza,Halima

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com