Uchaguzi wa Hong Kong kuahirishwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 31.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Uchaguzi wa Hong Kong kuahirishwa

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam anatarajiwa hii leo kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa bunge la mji huo wa Septemba 6, kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam anatarajiwa hii leo kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa bunge la mji huo wa Septemba 6, kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Uamuzi huo utakuwa pigo kwa upande wa upinzani unaopigania demokrasia Hong Kong, ambao ulikuwa na mataumaini ya kushinda wingi wa viti bungeni.

Unafanyika katika kipindi cha shera mpya na kali ya usalama

Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza tangu China ilipotangaza sheria mpya ya usalama wa kitaifa, ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha jela. China imesema sheria hiyo itatumika dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchochezi, njama za kujitenga, ugaidi na uingiliaji kati wa mataifa ya kigeni.

Soma zaidi: China yasitisha ushirikiano wa kisheria kati ya HK na nchi kadhaa

Serikali Kuu ya China na ya Hong Kong zimesema sheria hiyo haitotumika kukandamiza uhuru wa raia wa Hong Kong, bali inahitajika kurejesha utulivu baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya vurugu ya mwaka jana ya kuipinga serikali.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com