Uchaguzi wa Hambourg | NRS-Import | DW | 25.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Uchaguzi wa Hambourg

Kama kweli walinzi wa mazingira wataunda serikali ya muungano pamoja na wahafidhina ndilo suala kuu magazetini hii leo

Meya Ole von Beust (mbele)na mgombea wa SPD Neumann

Meya Ole von Beust (mbele)na mgombea wa SPD Neumann


Mada moja tuu ndio iliyowashughulisha mno wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo:Matokeo ya uchaguzi wa Hambourg.


Chama cha Christian Democratic Union CDU japo kama kimepoteza wingi mkubwa wa viti,lakini kinasalia kua chama kikuu katika bunge la mjini Hambourg.Maajabu yamezushwa na chama cha mrengo wa shoto Die Linke kilichofanikiwa kuingia bungeni.Matokeo ya uchaguzi huo yanapimwa kwa jicho tofauti na wahariri wa humu nchini.Gazeti la "Die FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND la mjini Hambourg linahisi:"Meya Ole Von BEUST anaweza kubadilisha mtindo wa kale wa kuunda serikali ya muungano.Wengi,tangu upande wa chama cha CDU na hata upande wa chama cha walinzi wa mazingira GAL wanaisubiri fursa hiyo.Na Hambourg inatoa nafasi nzuri ya jaribio kama hilo.Katika mji huo wa kaskazini,kawaida nadharia ya kisiasa haipewi umuhimu mbukwa sana kama katika majimbo mengine ya shirikisho.


Kuwakilishwa chama cha mrengo wa shoto Die Linke katika bunge la shirikisho na katika mabunge ya majimbo hakujasaidia bado kuupanua uwezekano wa kuunda muungano wa vyama vingi-kinyume kabisa-hali hiyo inachangia kuendeleza muungano uliopo au kama hakuna njia nyengine ,kukimbilia kuunda muungano wa vyama vikuu-chaguo ambalo mara nyingi linajitokeza kua ni baya zaidi.Serikali ya kwanza ya muungano wa chama cha CDU na walinzi wa mazingira inaweza kusaidia kuikwamua hali ya mambo na kugeuka mfano kwa majimbo mengine pia ya shirikisho.


Gazeti la NEUE DEUTSCHLAND la mjini Berlin linaandika:


"Kwamba Die Linke kitawakilishwa katika bunge la kumi kati ya 16 ya majimbo ya Ujerumani,hakuna aliyekua akishiku,sawa na vile ambavyo watu wanabidi kukubali kwamba chama hicho kimeshavuka mpaka na kuingia pia katika mabunge ya magharibi,hata kama hakipewi umuhimu mkubwa hivyo.


Gazeti la DIE WELT la mjini Berlin linaandika:


"Walinzi wa mazingira walisemekana wangemezwa na Die Linke waliokadiriwa kujikingia asili mia kumi.Matokeo yamekuja kua mengine kabisa.Pengine kauli ya mwenyekiti wa chama cha SPD KURT BECK ya kuwepo aina fulani ya ushirikiano pamoja na Die Linke ndio iliyowazindua wapiga kura wa walinzi wa mazingira.Hambourg ni mji wa wananchi na hivyo ndivyo uchaguzi ulivyokua.Kilichosalia ni kutaraji tuu kwamba CDU na GAL watakiuka kizingiti na kuunda serikali ya kwanza ya muungano wa aina hiyo.


►◄

 • Tarehe 25.02.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DCt5
 • Tarehe 25.02.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DCt5
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com