Uchaguzi wa bunge wafanyika leo Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 18.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Uchaguzi wa bunge wafanyika leo Pakistan

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema leo nchini Pakistan kuwapa nafasi wapakistan kushiriki katika uchaguzi wa bunge.

Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi uliopita lakini ukaahirishwa kufuatia kuuwawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan Benazir Bhutto mnamo tarehe 27 mwezi Disemba mwaka jana.

Usalama umeimarishwa hii leo kufuatia mashambulio kadhaa yaliyotokea wakati wa kampeni za uchaguzi huo Jumamosi iliyopita shambulio lililofanywa na mtu wa kujitoa muhanga dhidi ya wafuasi wa chama chake marehemu Benazir Bhutto liliwaua watu 47 katika mji mmoja ulio karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanistan.

Rais Pervez Musharraf wa Pakitan anasema uchaguzi wa leo ni hatua muhimu kuelekea utawala wa demokrasia kamili nchini humo.

Lakini viongozi wa chama cha Pakistan People´s Party, PPP na chama cha waziri mkuu wa zamani, Nawaz Sharif, cha Pakistan Muslim League, wanasema wanaamini uchaguzi huo hautakuwa huru wala wa haki.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com