1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Urusi

W.Alexander / R. Ali29 Novemba 2007

Jumapili hii warusi wanapiga kura lulichagua Duma-bunge. Uchaguzi wa Rais utakua Machi 2,2008

https://p.dw.com/p/CUgL
Rais Vladimir Putin wa Urusi akitoka hotuba katika televisheni
Rais Vladimir Putin wa Urusi akitoka hotuba katika televisheniPicha: AP

Wananchi wa Russia, wanakwenda kupiga kura jumapili hii.Kila mahala nchini Russia, zimezagaa picha za rais Putin na biramu lisemalo:“Mpango wa Putin ni ushindi kwa Russia.”Putin binafsi, ameueleza uchaguzi huu ni wa kuamua hatima ya Russia na hakuchoka kuonya juu ya maadui tangu wa ndani hata wa nje ya Russia.

Wapinzani wachache wanaothubutu kulalamika hadharani,hula mkomoto na kutiwa kizuizini.Wachunguzi wa kimataifa kutoka shirika la OSZE, wamenyimwa viza kuingia Russia.Lakini, warusi wanachagua nini na nani ?

Bunge la Russia Duma, si bunge halisi kwa tafsiri ya demokrasia ya magharibi .Labda ingefaa kulinganisha na bunge la iliokua Ujerumani mashariki (GDR) “Volkskammer”.Katika Bunge lile hakuna kujadiliana motomoto ,bali maazimio ya viongozi hupitishwa bila kuhojiwa au kupingwa.

Hali ni sawa na hiyo upande wa vyama vya kisiasa nchini Russia chini ya Putin.Hata katika Bunge la Ujerumani Mashariki –GDR, kulikuwapo na vyama vya kubabaisha -mfano wa chama cha kiliberali.Vyama hivi vikipaswa kufuata nyayo za chama-tawala cha SED.

Kufanya kila mmoja au kila chama kinatii,shirika la usalama la STASI lilikuwa macho.Katika Russia chini ya rais Putin chama-tawala pekee ni “Russia moja.”

Tofauti kati ya Russia ya leo na iliokua Ujerumani mashariki, iko katika nadharia.Russia leo haiegemei nadharia na wala haina programu nyengine isipokua Putin mwenyewe.

Hii ndio maana uchaguzi ujao umetangazwa na Kremlin kuwa ni kama “§kura ya maoni” wananchi kuamua iwapo wanamkubali rais Putin au la.Kusema kweli, Putin hata si mwanachama wa chama hiki.juu ya hivyo,amejichukulia nafasi 3 za kwsanza katika orodha yake ya kugombea uchaguzi.Russia nzima chama hiki cha “Russia moja” kimeeneza mabiramu yake yanayodai “Mpango wa Putin ndio ushindi kwa Russia nzima”.

Kiroja cha mambo ni kwamba huo mpango wa Putin ambao wapigakura wauidhinishe jumapili hii,haupo kabisa.Hakuna alieuona na wala hata Putin mwenyewe na anaungama hayo.

Isitoshe, katiba ya Russia,inamzuwia rais Putin kugombea tena uchaguzi wa rais hapo machi 2,mwakani.Na binafsi amekariri tena na tena kwamba, ataheshimu katiba.Kwahivyo, kuna faida gani kwa rais kupiga debe katika uchaguzi wa wabunge ?

Isipokuwa ,Putin anapanga kuton’gatuka.Anapanga kubakia alao katika wadhifa fulani usiofahamika.

Putin aliishi katika ile iliokua Jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani au Ujerumani Mashariki (GDR).Miaka yake aliopitisha huko akiwa jasusi wa shirika la KGB,ameieleza ndio ya furaha maishani mwake.Kwa bahati mbaya Ujerumani Mashariki hakujakuwa na mafuta ya petroli.Nchini Russia lakini,yamejaa tele.Russia chini ya Putin, kwa muujibu wa shirika la “TRANSPERENCY INTERNATIONAL” -shirika linalopiga vita ufisadi,ndio nambari one katika ulaji-rushua.

Kwahivyo, desemba 2,jumapili hii ijayo, warusi wanakipigia kura kitu gani au nani ?

Wanalichagua Bunge la taifa Duma ambalo halina zaidi ya kusema isipokuwa kuitikia amini kama lile la iliokua JKU-Volkskammer.Au wanampigia tu kura Putin .