UChaguzi umeanza Ufaransa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

UChaguzi umeanza Ufaransa

PARIS:

Uchaguzi pia umeanza leo kumchagua rais mpya wa Ufaransa:

Vituo vya uchaguzi vimefunguliwa tayari leo kuanza kupiga kura katika visiwa vidogo vya Ufaransa vya Saint Pierre na Miquelon,karibu na Kanada.Ni wapiga kura 50000 huko wamesajiliwa kupiga kura.

Kesho kiasi cha wsapigakura milioni 44.5 watamchakua mrithi wa kiti cha rais wa sasa Jacques Chirac katika duru 2 za uchaguzi-kesho na Mei 6.

Katika jumla ya watetezi 12 wa duru ya kesho mhafidhina Nicolas Sarkozy yupo takriban bega kwa bega na msoshalisti Bibi Segolene Royal.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com