Uchaguzi nchini Msumbiji | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 31.10.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Uchaguzi nchini Msumbiji

Rais Armando Guebuza anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais na bunge nchini Msumbuji.

Rais Armando Guebuza akipiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge nchini Msumbiji siku ya Jumatano , mjini Maputo, Oct. 28, 2009.

Rais Armando Guebuza akipiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge nchini Msumbiji siku ya Jumatano , mjini Maputo, Oct. 28, 2009.

MAPUTO:

Nchini Msumbiji, Rais Armando Guebuza na chama chake cha Frelimo wanaongoza katika chaguzi za rais na bunge. Baada ya kuhesabiwa nusu ya kura zilizopigwa,Guebuza amejikingia asilimia 78 ya kura hizo na chama chake asilimia 77.

Chama cha Frelimo kilitazamiwa kushinda tangu hapo awali kwa sababu upande wa upinzani una mivutano. Hata Guebuza ametarajiwa kuchaguliwa tena. Hii itakuwa awamu yake ya pili madarakani. Chama cha Frelimo kinatawala tangu Msumbiji ilipopata uhuru wake kutoka Ureno katika mwaka 1975.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa rasmi tarehe 12 Novemba.

 • Tarehe 31.10.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KJgr
 • Tarehe 31.10.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KJgr
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com