1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Guinea Bissau mtafaruku mtupu

Mohammed Khelef
25 Novemba 2019

Uchaguzi wa rais nchini Guinea Bissau uliofanyika jana (25 Novemba) umemalizika kwa mparaganyiko baada ya kambi ya Rais Jose Mario Vaz kuwatuhumu wapinzani kufanya udanganyifu.

https://p.dw.com/p/3TgQN
Portugal Universität Lissabon | Jose Mario Vaz, Präsident Guinea-Bissau
Picha: DW/J. Carlos

Uchaguzi wa rais nchini Guinea Bissau uliofanyika jana umemalizika kwa mparaganyiko baada ya kambi ya Rais Jose Mario Vaz kuwatuhumu wapinzani kufanya udanganyifu kwenye upigaji kura na kuzuka vurugu kwenye taifa hilo la magharibi ya Afrika ambalo huandamwa na mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara.

Uchaguzi wa jana ulihitimisha miaka minne ya machafuko ya kisiasa chini ya rais Vaz ambaye mara kwa mara aliwafuta kazi mawaziri wake wakuu na kuingia kwenye mzozo na bunge.

Licha ya kutoa ahadi ya kukubali matokeo, kambi ya Vaz imewatuhumu mahasimu wake wa muda mrefu kwa kufanya udanganyifu kwenye uchaguzi huo na wameashriia kuyakataa matokeo yake.

Vaz na chama cha PAIGC, ambacho ni kikubwa ndani ya bunge wamekuwa kwenye mvutano tangu mwaka 2015 juu ya nani anapaswa kuiongoza serikali hali iliyosababisha mkwamo wa kisiasa nchini Guinea Bissau.