Ubepari watoweka polepole | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.02.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ubepari watoweka polepole

Hiyo jana, maelfu ya watu waliandamana barabarani katika mji mkuu wa Senegal, Dakar kuadhimisha ufunguzi wa kongomano la kijamii la kimataifa linalofanywa kila mwaka.

Senegalese women carry signs with the names of the country's different regions and a banner calling for the preservation of land rights as they walk in a march on the opening day of the World Social Forum in Dakar, Senegal Sunday, Feb. 6, 2011. The anti-capitalist gathering that serves as an annual counterweight to the World Economic Forum kicked off in Senegal on Sunday with a march and a speech by Bolivian President Evo Morales. (AP Photo/Rebecca Blackwell)

Wanawake watoa wito kuhifadhi haki za kumiliki ardhi

Hadi Februari 11, kongomano hilo linalopinga utandawazi litajadili mzozo wa sera za kibepari na kutafuta njia mbadala. Kongomano hilo ambalo ni maarufu kama mpinzani wa ubepari, linafanyika barani Afrika kwa mara ya pili. Hadi wajumbe 50 elfu, wanatazamiwa kushiriki katika kongomano la mwaka huu kujadili mzozo wa ubepari. Kwa wapinzani wengi wa utandawazi, waliokwenda Dakar, mkutano huo nchini Senegal una umuhimu mkubwa kwani unafanyika barani Afrika. Mmauritania, Babouna Khalifa D'Akite anaishi Dakar tangu miaka mingi, anasema:

" Waafrika watatoa malalamiko yao kwenye kongmano hilo - hasa kupigania hali bora ulimwenguni na kudhihirisha matatizo yanayokabiliwa na bara la Afrika."

Yeye anatetea haki za wakimbizi waliotokea nchini mwake na kwa maoni yake ni muhimu sana kwa kongomano hilo kujadili pia matatizo yanayohusika na uhamiaji. Kwa vile mwaka huu mkutano huo unafanyika nchini Senegal, midahalo mingi itahusika na kile kilichoitwa, mzozo wa ubepari uliozagaa barani Afrika na sehemu zingine ulimwenguni.

Mghana, Philip Kumah anaefanyakazi na Amnesty International, shirika linalogombea haki za binadamu duniani, anasema kuwa wanachotaka ni kuona mwisho wa dhulma nchini mwao, ambako jamii zinanyanganywa ardhi na serikali. Kongomano hilo linatoa fursa kwa serikali kusikiliza malalamiko ya wananchi wake.

Boliviens Präsident Evo Morales auf dem Weltsozialforum 2011. Weltsozialforum 2011, Dakar, Senegal, Afrika Aufnahmedatum: 6.2.2011. Copyright Renate Krieger/DW.

Rais Evo Morales wa Bolivia katika Kongomano la Kijamii la Kimataifa, mjini Dakar

Lakini hadi sasa, kongomano la kijamii la kimataifa limegubikwa na mada nyingine - maandamano ya upinzani yanayoendelea nchini Misri na yaliyotokea Tunisia mwezi uliopita. Hiyo jana mjini Dakar, maandamano ya wapinzani wa utandawazi wapatao kama elfu 20 hadi 30, yaliishia mbele ya Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop. Huko jukwaani, Rais wa Bolivia Evo Morales alitoa mwito kwa viongozi wenzake kushiriki katika kongomano hilo. Alisema, ubepari hutoweka polepole, pale unapokabiliwa na upinzani. Matukio ya nchini Misri na Tunisia ni ishara za mageuzi.

Hii leo rais wa Senegal, Abdoulaye Wade anakutana na wajumbe wa makundi yenye sera za mrengo wa kushoto kutoka kila pembe ya dunia. Miongoni mwao ni rais wa zamani wa Brazil, Lula da Silva. Hata rais Alpha Conde wa Guinea anatazamiwa kushiriki katika kongomano la mjini Dakar litakalomalizika February 11.

Mwandishi:Krieger,Renate /ZR/Martin,Prema
Mpitiaji:Abdul-Rahman,Mohammed

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com