1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubelgiji yabaki tena bila serikali.

2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVeu

Brussels. Yves Leterme , ambaye aliteuliwa kuunda serikali nchini Ubelgiji na kuwa waziri mkuu, amejiuzulu mamlaka yake, baada ya kushindwa kuleta maelewano kutokana na mpasuko wa kisiasa baina ya watu wanaozungumza lugha ya Flemish na wale wanaozungumza lugha ya Kifaransa nchini humo. Kujiuzulu kwake kunakuja baada ya mmoja kati ya washiriki muhimu wa kuunda serikali ya mseto kukataa kuunga mkono mpango wa kuwa na uhuru zaidi katika kambi hizo mbili.

Mfalme Albertz 11 amekubali kujiuzulu huko kwa kiongozi anayetoka upande wa wanaozungumza lugha ya Kiflemish wa chama cha Christian Democratic. Ubelgiji imekuwa bila ya serikali sasa kwa muda wa siku 174.