1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubalozi wa Ufaransa wafunguliwa tena nchini Libya

Amina Mjahid
30 Machi 2021

Ufaransa imeufungua tena ubalozi wake nchini Libya baada ya kufungwa kwa miaka saba. Ubalozi huo ulifunguliwa jana Jumatatu ikionesha ishara ya kuanza kurejea amani na utulivu nchini Libya. 

https://p.dw.com/p/3rMyp
Frankreich Präsident Emmanuel Macron
Picha: Lewis Joly/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza juu ya  kufunguliwa tena ubalozi huo wiki iliyopita alipokutana kwa mazungumzo mjini Paris na Rais wa baraza la serikali ya mpito ya Libya, Mohamed al-Manfi aliyeingia madrakani hivi karibuni.

Libya ilitumbukia kwenye machafuko baada ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gadhafi kuangushwa na kuuawa.

soma zaidi: Libya yapata serikali ya mpito

Wanadiplomasia na raia wa kigeni wengi waliondoka katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika baada ya kuwepo visa vya mashambulio ya mara kwa mara na utekaji nyara, moja wapo likiwa lile la kushambuliwa ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa mashariki wa Benghazi mnamo Septemba mwaka 2012 ambapo balozi Chris Stevens na Wamarekani wengine watatu waliuawa.

Nchi nyingine zinazotarajiwa kufungua tena balozi zake ni pamoja na Misri, Ugiriki na Malta. Italia iliufungua ubalozi wake mjini Tripoli tangu mwaka 2017.