Ubalozi wa Israel nchini Misri, washambuliwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.09.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ubalozi wa Israel nchini Misri, washambuliwa

Waziri Mkuu wa Misri ameitisha kikao cha dharura cha baraza la mawaziri baada ya waandamanaji kuushambulia ubalozi wa Israel mjini Cairo jana usiku na kutupa mamia ya nyaraka za ubalozi huo.

default

Waandamanaji nchini Misri

Balozi wa Israel nchini Misri ameripotiwa kuondoka nchini humo mapema leo, kurejea nyumbani.

Rais Barack Obama wa Marekani ameitaka Misri kuulinda ubalozi huo dhidi ya waandamanaji na katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameeleza wasiwasi wake kuhusu tukio hilo.

Mamia ya polisi na wanajeshi wamepambana na waandamanaji ambao jana usiku, waliuvunja uzio unaozunguka jengo la ubalozi wa Israel mjini Cairo. Uzio huo ulijengwa na serikali ya Misri baada ya maandamano kufanywa kila siku nje ya ubalozi wa Israel, kupinga mauaji ya walinzi watano wa mpakani wa Misri, katika mji wa Sinai.

Erneute Gewalt zwischen Israel und Palästinensern August 2011

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, akimjulia hali mmoja wa majeruhi katika ghasia zilizotokea mpakani mwa nchi hiyo na Misri

Walinzi hao waliuawa kwenye mpaka wa Misri, katika shambulio la Israel lililowalenga wapiganaji wa Kipalestina.

Kufuatia ghasia hizo za waandamanaji mjini Cairo, Misri imetangaza tahadhari ya hali ya juu.

 • Tarehe 10.09.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12WUa
 • Tarehe 10.09.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12WUa

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com