Uamuzi wa kufanyika uchaguzi utafanyika Jumanne. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Uamuzi wa kufanyika uchaguzi utafanyika Jumanne.

Islamabad. Tume ya uchaguzi nchini Pakistan imesema kuwa uamuzi iwapo uchaguzi wa bunge utafanyika kama ulivyopangwa hapo Januari 8 ama la utatangazwa leo Jumanne. Maafisa wa ngazi ya juu wa serikali, hata hivyo wamesema kuwa huenda uchaguzi huo ukaahirishwa kwa muda wa wiki kadha. Siku ya Jumapili chama cha Pakistan Peoples Party kimemteua mtoto wa kiume na mume wa kiongozi aliyeuwawa Benazir Bhutto kuchukua nafasi yake. Bilawal Bhutto Zardari ana umri wa miaka 19 akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza. Ameteuliwa rasmi kuwa mwenyekiti wa chama cha PPP, wakati baba yake Asif Ali Zardari, atachukua kazi ya kukiendesha chama hicho. Nae waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Shariff, ambaye hapo kabla alitoa wito wa kususiwa uchaguzi wa hapo Januari, amesema kuwa chama chake kimeamua kushiriki katika uchaguzi.

Baada ya majadiliano na wanachama wa chama chetu asubuhi ya leo na jana usiku, tumeamua kugombea katika uchaguzi ujao.

Zaidi ya watu 40 wameuwawa katika ghasia ambazo zimefuatia kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto baada ya mkutano wa kampeni ya uchaguzi mjini Rawalpindi Alhamis iliyopita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com