1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UAE yasitisha zoezi la kutoa visa kwa raia wa nchi 13

Zainab Aziz
25 Novemba 2020

Utawala wa Falme za Kiarabu umesimamisha zoezi la kutoa visa kwa watu kutoka mataifa 13 yenye raia wengi wa Kiislamu. Je ni kwa nini?

https://p.dw.com/p/3louG
UAE Visa-Amnesty für Gastarbeiter in Sicht
Picha: picture-alliance/AP-Photo/K. Jebreili

Miongoni mwa nchi hizo ni Iran, Syria, Somalia, Afghanistan, Yemen na Libya kwa mujibu wa taarifa ya serikali. Marufuku hiyo pia imezikumba nchi za Kenya, Algeria, Irak, Lebanon, Pakistan, Tunisia na Uturuki. Uamuzi huo utatekelezwa hadi itakapoamulia vinginevyo na haikuelezwa iwapo

Taarifa hiyo, inayonukuu idara ya uhamiaji imetolewa kwa kampuni mbalimbali na imeashiria kuwa agizo hilo lilianza kutumika tangu tarehe 18 mwezi huu wa

Chanzo kimoja kimefahamisha shirika la habari la Reuters kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu umechukua hatua hiyo kutokana na wasiwasi wa kiusalama ijapokuwa chanzo hicho hakikutaja wasiwasi wenyewe kwa kirefu. Hata hivyo shirika la habari la Reuters limefahamishwa kuwa marufuku hiyo itakuwepo kwa kipindi kifupi tu.

Wiki iliyopita, wizara ya mambo ya nje ya Pakistan ilisema Umoja wa Falme za Kiarabu ulisitisha utoaji wa viza kwa raia wake nan chi nyinginezo nchini humo na imekuwa inataka kupewa taarifa zaidi au sababu ya kusimamishwa zoezi hilo lakini pia imekuwa ikifikiria huenda hatua hiyo imetokana na janga la corona.

Pakistan kwa upande wake imefahamisha kwamba raia wake walio na viza za Umoja wa Falme za Kiarabu hawatoathiriwa na vikwazo hivyo vipya.

Chanzo: Reuters