Twaweza: Polisi Tanzania yaongoza kwa rushwa | Matukio ya Afrika | DW | 22.11.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Twaweza: Polisi Tanzania yaongoza kwa rushwa

Idara ya polisi na mahakama Tanzania zinaongoza kwa rushwa kulingana na ripoti ya utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza.

Utafiti wa shirika lisilo la kiserikali la Twaweza nchini Tanzania umebaini kuwa idara za polisi na mahakama bado zinaongoza kwa rushwa, licha ya kuwa kwake taasisi zinazohudumia idadi kubwa ya watu. Hayo yamesemwa kwenye uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina "Hawashikiki" uliofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kutoka sekta za umma na kibinafsi.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, wananchi wanaripoti kuwa licha ya viwango vya rushwa kupungua nchini kwa mwaka huu, bado idara za polisi na mahakama zimeendelea kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa. Kati ya asilimia thelathini na sita na thelathini na tisa ya wananchi waliohojiwa, wameiambia Twaweza kuwa waliombwa rushwa mara ya mwisho walipofika katika taasisi hizo.

Hata hivyo mkurugenzi meneja utetezi wqa TWAWEZA, Anastazia Lugaba, amesema kuwa wananchi walitoa rushwa ili kupata huduma ya uhakika katika sekta hizo lakini kwa sauti za wananchi zinazoonesha matumaini katika mapambano dhidi ya rushwa.

Rushwa katika sekta ya madini

Ndani ya utafiti huo pia wananchi wamezungumzia sakata maarufu la kampuni ya madini ya Accacia wakiliweka katika kundi la rushwa kutumika kwa kiasi kikubwa, huku Mamlaka ya Mapato ya Tanzania pamoja na Mamlaka ya Bandari nazo zinaonekana kushughulikiwa ipasavyo na Mamlaka ya Kushughulikia Rushwa hapa nchini TAKUKURU, huku wakitaja vyama vya upinzani vingelifanya vizuri zaidi katika kupambana na rushwa endapo vingepata nafasi ya kuwa mamlakani.

Idara za polisi na mahakama zimeendelea kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa

Idara za polisi na mahakama zimeendelea kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa

Taasisi ya kupambana na rushwa nchini TAKUKURU wameukubali utafiti huo uliofanywa mwezi Agosti mwaka huu kwa kusema kuwa malalamiko ya rushwa yanaongezeka kwa kasi kwa tafsiri kuwa ujasiri miongoni mwa wananchi, chuki dhidi ya rushwa pamoja na uwelewa juu ya rushwa ndio hufanya malalamiko hayo kuongezeka.

Wanachi wataka hatua zaidi kuchukuliwa


Wananchi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali wameiambia Dw kuwa, licha ya kuona vigogo mbalimbali wakipandishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma za rushwa zinazowakabili, ni hatua muhimu ambayo serikali inaweza kujivunia kwa katua hiyo.

Katika utafiti huo wananchi wengi wamependekeza wote wanaopatikana na hatia za rushwa wafungwe gerezani na kufutwa kazi kabisa, hii ni adhabu iliochaguliwa zaidi kwa askari wa barabarani, afisa ardhi kwa serikali za mitaa pamoja na wanansiasa, na kuongeza kuwa rushwa kubwa zipewe kipaumbele katika mapambano dhidi ya rushwa.

Mwandishi: Hawa Bihoga
Mhariri: Mohammed Khelef