Tuzo ya mashika ya wachapisha vitabu ya Ujerumani atunukiwa Friedländer | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tuzo ya mashika ya wachapisha vitabu ya Ujerumani atunukiwa Friedländer

Frankfurt Am Main:

Mtaalam wa Taareh wa Israel,Saul Friedländer ametunukiwa hii leo zawadi ya amani ya shirika la wachapisha vitabu nchini Ujerumani.Mtaalam huyo wa historia mwenye umri wa miaka 75 amekabidhiwa tuzo hiyo yenye thamani ya yuro 25 elfu katika kanisa la Paul mjini Frankfurt.Friedländer anaeishi nchini Marekani,amepata umashuhuri mkubwa kutokana na kitabu chake „Enzi ya tatu na wayahudi“ akichambua mauwaji ya halaiki ya wayahudi yaliyofanywa na wanazi katika vita vikuu vya pili vya dunia Holaucust

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com