Tuzo kwa habari za kuwakamatisha wauaji | Habari za Ulimwengu | DW | 20.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tuzo kwa habari za kuwakamatisha wauaji

SANAA: Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemen itatoa tuzo ya kama Euro 50,000 kwa habari zitakazowakamatisha washambulizi walioua watalii 2 wa Kibeligiji.Madreva 2 wa Kiyemeni pia waliuawa baada ya basi la watalii kushambuliwa na watu waliokuwa na bunduki.Mauaji hayo yalitokea karibu na mji wa kihistoria wa Shibam nchini Yemen.Watalii wengine 12 wa Kibeligiji walionusurika,sasa wamesharejea Ubeligiji.

Kwa mujibu wa serikali ya Yemen,mashambulizi hayo huenda ikawa yalifanywa na Al Qaeda.Tawi la Al Qaeda nchini Yemen,limeapa kufanya mashambulizi kadhaa nchini humo kwa azma ya kuishinikiza serikali kuwaachilia huru wanamgambo waliofungwa jela nchini Yemen.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com