1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tunisia yatangaza kuunda baraza jipya la mawaziri

Amina Mjahid
2 Januari 2020

Waziri Mkuu mteule wa Tunisia Habib Jemli ametangaza kuunda bazara jipya la mawaziri linalojumuisha wataalamu wasiohusiana na vyama

https://p.dw.com/p/3VbEY
Tunesien Amtseid Parlamentsmitglieder in Tunis
Picha: Reuters/Z. Souissi

Hatua hii inajiri mwezi mmoja tangu kuchaguliwa kuiongoza serikali ya nchi hiyo huku lengo kuu likiwa ni kuufufua uchumi ulioporomoka. Jemli, amesema serikali mpya itajumuisha raia wa Tunisia wanaotoka nje ya nchi, bila ya kuwataja kwa majina.

Shirika la habari la TAP la nchini humo, limesema Jemli atawasilisha majina hayo kwa Rais Kais Saied ambaye ataliomba bunge kuandaa kikao maalumu cha kulipigia kura ya imani baraza hilo jipya lilopendekezwa.

Baraza hilo la mawaziri litahitaji kuidhinishwa kwa kura 109 katika bunge lenye viti 217.