1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume huru kuchunguza matokeo ya uchaguzi wa Kenya

16 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D8VD

NAIROBI:

Serikali ya Kenya na wajumbe wa chama kikuu cha upinzani wamekubaliana kuunda tume huru itakayochunguza mgogoro wa matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka jana uliomrejesha madarakani Rais Mwai Kibaki.Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anaongoza majadiliano ya upatanisho kati ya serikali na chama kikuu cha upinzani ODM cha Raila Odinga.

Annan amesema,masuala yanayojadiliwa ni magumu lakini kuna maendeleo yaliyopatikana.Hata hivyo ni mataumaini yake kuwa pande hizo mbili hivi karibuni zitakubaliana kuunda serikali ya mseto.Majadiliano hayo ya upatanisho yataanza tena Jumanne ijayo.

Matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanywa Desemba 27,ambayo upinzani unasema yamefanyiwa udanganyifu,yalizusha mapambano makali ya kikabila nchini Kenya. Zaidi ya watu 1,000 waliuawa katika machafuko hayo na maelfu wengine wamepoteza makaazi.