Tukio 26 – Kumuaga Ayhan | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 26 – Kumuaga Ayhan

Hali ya huzuni imetanda katika afisi za Radio D. Ayhan anawaaga wenzake na anarudi nchini Uturuki. Ingawa wafanyikazi wenzake wamemwandalia hafla ya kumuaga, hawana la kuchangamkia.

Wafanyikazi wenzake hawana budi ila kumuaga Ayhan.

Wafanyikazi wenzake hawana budi ila kumuaga Ayhan.

Paula anafika kazini asubuhi na kuwapata watu wote wakijitayarisha kwa sherehe. Hafurahii sherehe hizo kamwe: Ayhan anaondoka Radio D kurudi zake Uturuki kumsaidia baba yake. Katika harakati za kumuaga Ayhan, wafanyi kazi wenzake wameandaa hotuba fupi na zawadi ya kumbukumbu ya rafiki yake Eulalia.

Kutokana na hafla hiyo ya kumuaga Ayhan, mwalimu hajishughulishi na sarufi. Hata hivyo anazungumzia maneno machache kuhusu nomino ambatani.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa