Tukio 23 – Pezi la Papa | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 23 – Pezi la Papa

Paula na Philipp wanategua kitendawili cha mahali pa kwenda kumwangalia papa na kwa mara nyingine tena wanagundua ulaghai uliohusika. Hata hivyo mwanzoni sababu za tukio hilo si dhahiri moja kwa moja.

Mpiga-mbizi alikuwa na lengo gani?

Mpiga-mbizi alikuwa na lengo gani?

Wakiwa katika harakati za kumtafuta mwanamichezo wa kuteleza baharini aliyetoweka, Paula na Philipp wanakutana na mpiga mbizi na hapo wanapata fununu. Mpiga mbizi alikuwa amewahangaisha nusu ya wakazi wa Hamburg kwa kujifunga pezi la papa mgongoni mwake. Wakati huo huo Eulalia amefika Hamburg tayari kusaidia. Pia naye amegundua kitu fulani.

Eulalia amepata fununu ambayo huenda ikawasaidia Paula na Philipp- fursa nzuri ya kutumia wakati timilifu. Zingatia zaidi jinsi ya kutumia wakati uliopita hali ya kwendelea.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa