Tukio 20 – Uchunguzi wa Wasikilizaji | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 20 – Uchunguzi wa Wasikilizaji

Paula na Philipp wanawataka wasikilizaji kutoa maoni yao. Mada ya kipindi ni, "Je kusema uongo ni dhambi?" Wasikilizaji wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maduara bandia ya mimea na tabia ya wakulima.

Wie halten es die Hörer mit dem Lügen?

Wie halten es die Hörer mit dem Lügen?

"Je kusema uongo ni dhambi?" Paula na Philipp wanawauliza wasikilizaji. Swali hilo limetokana na matukio kwenye shamba la mahindi ambayo waandishi habari hao waliyatangaza. Je wakulima walaumiwe kwa vitendo vyao au watalii wanapaswa kujilaumu wenyewe kwa ujinga wao? Wasikilizaji wanaeleza mambo kinagaubaga.

Tofauti na waandishi habari ambao wanauliza wasikilizaji maswali ya kujibu "ndiyo" au "la", mwalimu anatoa jukumu lenye uwezekano wa kushughulikiwa kwa jinsi tatu. Nomino za kijerumani zimo katika jinsia tatu: jinsia ya kiume, jinsia ya kike au bila jinsia. Haya yameelezwa katika tukio hilo pamoja na matumizi ya vidhihirisho "der," "die" na "das."

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa