Tukio 18 – Uchunguzi wa Usiku | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 18 – Uchunguzi wa Usiku

Paula na Philipp wanataka kujua mbivu na mbichi kuhusu maumbo ya duara ya mimea na wanakwenda usiku kuchunguza. Lakini wanachokumbana nacho hakihusu viumbe kutoka angani.

Ni nini kinachoendelea usiku kwenye shamba la mahindi?

Ni nini kinachoendelea usiku kwenye shamba la mahindi?

Mwenye shamba lenye maumbo ya duara yasiyoeleweka anawatoza watalii ada ya Yuro 5 kila mmoja ili wapige picha maumbo hayo. Wakati huo huo Philip na Paula wamepiga kambi mwituni kusubiri madude yanayoanguka kutoka angani. Badala yake, wanaume wawili wanajitokeza wakiwa na mtambo. Je wao ndio waliotayarisha hayo maduara ya mimea kuwavutia watalii? Hatimaye, dude kutoka angani linaonekana na hivyo kuzidisha kizungumkuti.

Kitenzi "machen" kinaeleweka kwa urahisi. Katika tukio hili mwalimu anakufunza namna tofauti za kutumia neno hili.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa