Tukio 17 – Maduara ya Mimea | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 17 – Maduara ya Mimea

Paula na Philipp wanakwenda kuchunguza wakati maumbo ya duara yanapogunduliwa kwenye shamba la mahindi. Je kuna dude lililoanguka kutoka angani au kuna mtu anawacheza watu shere?

Hakuna anayejua asili ya maumbo ya duara.

Hakuna anayejua asili ya maumbo ya duara.

Wakati Ayhna anapowasili katika afisi ya Radio D, nao Paula na Philipp wamo njiani kutoka afisini. Maumbo ya duara yamegunduliwa katika shamba la mahindi na hakuna anayeweza kueleza jinsi yalivyojitokeza. Si waandishi habari hao wawili pekee walio na hamu ya kushuhudia jambo hilo; watalii wengi wanakuja kushuhudia pia. Wakazi wa kijiji hicho wanapata namna ya kujifaidi kutokana na tukio hilo la ajabu.

Katika zogo hilo, watu wenye nia tofauti wanajumuika. Watalii wana hamu ya kujionea wenyewe, waandishi habari wanataka kuagua kitendawili hicho na wakulima wanataka kufaidika kifedha. Zingatia vitenzi vya utaratibu katika tukio hili.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa