Tukio 16 – Ikarus | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 16 – Ikarus

Waandishi wote wawili wanashangazwa na kisa cha tanzia cha Ikarus, shujaa wa visaasili vya Kigiriki. Paula na Philipp wanaeleza kisa chake.

Ikarus hakuzingatia ushauri wa baba yake.

Ikarus hakuzingatia ushauri wa baba yake.

Paula na Philipp wanapomwona mvulana mdogo amevaa vazi la Icarus wanaingiwa na fikra: Wanaamua kukizungumzia kisa hicho cha Kigiriki kwenye mmoja wapo wa michezo yao ya redio. Kisa chenyewe ni kumhusu kijana ambaye hakufuata nasaha ya baba yake Daedalus na anaanguka anapojaribu kupaa angani. Amezidiwa na tamaa ya kulikaribia jua lakini anapolikaribia nta iliyo kwenye mbawa zake inaanza kuyeyuka.

"Usipae juu sana, na usishuke chini sana," Daedalus anamwambia mwanawe Ikarus. Kitenzi cha amri, kilichoshughulikiwa katika tukio hili, kinaweza kutumiwa, kuomba, kuamuru, kuonya au kuagiza. Lau Ikarus alimsikiliza baba yake, pengine hangeanguka.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa