Tukio 15 – Mavazi ya Karnivali | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 15 – Mavazi ya Karnivali

Paula na Philipp wanatangaza mara nyingine tena kuhusu Karnivali kutokea barabarani. Wanatambua mavazi tofauti na pia wanajifunza lahaja chache za Kijerumani katika harakati za kazi yao.

Wanawake hukata tai za wanaume wakati wa Karnivali katika maeneo yanayokaribia Mto Rhein.

Wanawake hukata tai za wanaume wakati wa Karnivali katika maeneo yanayokaribia Mto Rhein.

Afisini Paula analipiza kisasi dhidi ya Ayhan- kwa kutumia taratibu za Karnivali. Kisha kwenye vifijo na nderemo zilizopo barabarani, Philipp na Paula wanatoa taarifa kuhusu mavazi ya asili wanayoyashuhudia. Wanapambana na Papageno kutoka kwenye opera ya Mozart "The Magic Flute" – "Zumari ya Kichawi", na Ikarus, shujaa wa visaasili vya Kigiriki.

Philipp na Paula wanakutana na watu wa maeneo mbali mbali ya Ujarumani, wanaozungumza kwa lahaja za kienyeji. Fungua kiungo kilicho chini upate mwongozo wa DW-WORLD.DE wa lahaja.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa