Tukio 13 – Jumatatu ya Karnivali | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 13 – Jumatatu ya Karnivali

Si watu wote wanaofurahia Karnivali. Kazi ya Compu inasababisha waandishi habari hao wawili kwenda Schwarzwald ambako Karnivali inachangamkiwa zaidi.

Paula si shabiki wa Karnivali.

Paula si shabiki wa Karnivali.

Katika baadhi ya maeneo ya Ujerumani watu wanasherehekea Karnivali kwa furaha kubwa. Katika afisi ya Radio D kuna sintofahamu kati ya wahudumu kuhusu sherehe hizo. Paula haoni la kumvutia hata aungane na Philipp kufurahia. Kwake yeye vazi la kichawi alilovaa Philipp ni kichekesho kikubwa.

Philipp anafurahia uchunguzi wao unapowaelekeza Schwarzwald ambako watu waliovaa mavazi ya kichawi wanaiba magari katika zaazaa linaloendelea la Karnivali. Waandishi habari hao wanajaribu kuwa na kipindi cha moja kwa moja cha redio lakini wanashindwa. Wachawi wanamteka nyara Philipp baada ya kumburura kutoka kwenye gari.

Mpangilio wa maneno katika Kijerumani si jambo la kuchanganya sana. Tukio hili linalenga nafasi ya kiima na kiarifu.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa