Tukio 10 – Mahojiano na Mfalme Ludwig | Radio D Teil 1 | DW | 24.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 10 – Mahojiano na Mfalme Ludwig

Philipp anakutana na mwigizaji anayeigiza nafasi ya Mfalme Ludwig katika onyesho la muziki na kumtaka afanye mahojiano naye. Ghafla anatambua sauti yake. Wakati huo huo mgeni asiyetarajiwa atembelea afisi ya Radio D.

Philipp amtambua 'mfalme'.

Philipp amtambua 'mfalme'.

Katika Kasri la Neuschwanstein, Philipp bila ya msaada wa Paula anafanikiwa kumtambua mtu huyo anayejidai ufalme: ni mwigizaji wa onyesho la muziki la Mfame Ludwig. Philipp anatumia fursa hiyo kumhoji mwanamume huyo. Anaporudi katika afisi ya Radio D mjini Berlin, anashangaa kumpata bundi anayeongea.

Tukio hili linaashiria maastajabu anayokumbana nayo Philipp. Utamsikia mara kadha akisema "Das glaube ich nicht" (Hilo siliamini) na "Das weiß ich nicht" (Hilo silijui). Hii ni fursa ya kuzingatia zaidi neno la kukanushia "nicht".

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa