Tukio 09 – Muziki wa Ludwig | Radio D Teil 1 | DW | 24.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 09 – Muziki wa Ludwig

Philipp pia anapata fununu ya kumtambua mgeni. Anaona tangazo gazetini la onyesho la muziki kumhusu Mfalme Ludwig. Akiwa njiani kwenda kwenye ukumbi, anawahoji watalii wanaozuru kutoka maeneo yote ulimwenguni.

Philipp apanda basi kwenda kwenye ukumbi wa sanaa.

Philipp apanda basi kwenda kwenye ukumbi wa sanaa.

Huku Paula akiwa afisini mwake Berlin, Philipp naye anahangaika huku na huko mjini Munich. Hana habari yoyote kuhusu jambo aliloligundua Paula, lakini hata hivyo naye anaendelea vyema na uchunguzi wake. Kwenye basi anapoelekea ukumbini anazungumza na watalii kuhusu wanalotarajia kutokana na onyesho la muziki.

Fanya mazoezi ya ufahamu wa kusikiliza katika tukio hili. Kwenye basi utasikia lugha nyingi zikizungumzwa. Jitahidi kutambua maneno ya Kijerumani. Utafahamishwa kuhusu neno la kukanushia "nichts" na mahali pake baada ya kitenzi.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa