Tukio 05 – Mfalme Ludwig bado yu hai! | Radio D Teil 1 | DW | 24.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 05 – Mfalme Ludwig bado yu hai!

Paula na Ayhan wanamkaribisha mfanyikazi mwenzao mpya katika Radio D. Tayari wana jukumu muhimu la kutekeleza. Marehemu Mfalme Ludwig wa Bavaria anasemekana angali hai na kundi hilo linataka kuchunguza kadhia hiyo.

Kazi ya kwanza imeshapangwa.

Kazi ya kwanza imeshapangwa.

Philipp anakutana na wafanyikazi wenzake wapya Paula na Ayhan, na pia Josefine ambaye anasimamia taratibu za afisini. Hapana muda wa kupoteza maana Philipp na Ayhan tayari wanajua habari yao ya kwanza. Kuna tetesi kwamba mfalme maarufu Ludwig wa Pili wa Bavaria angali hai, ingawa alisemekana alifariki kwa njia isiyoeleweka mwaka 1886. Waandishi habari hao wawili wanaelekea katika Kasri la Neuschwanstein kuchunguza na kujifahamisha.

Mambo yasiyoeleweka yanazua maswali mengi. Katika tukio hili unaweza kufahamu zaidi maneno ya kuulizia maswali na majibu.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa