Tukio 02 – Simu kutoka Radio D | Radio D Teil 1 | DW | 24.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 02 – Simu kutoka Radio D

Philipp hajapata amani yoyote wala utulivu. Baada ya kusumbuliwa na wadudu, inambidi kukabiliana na majirani wasioisha kelele. Anapopigiwa simu asiyoitarajia kutoka Berlin, anaondoka haraka.

Habari njema kwa Philipp

Habari njema kwa Philipp

Usumbufu aliopata kutokana na wadudu si lolote si chochote! Maji yanamfika shingoni Philipp anapokabiliana na kelele za msumeno wa umeme pamoja na mpiga tarumbeta limbukeni. Paula kutoka Radio D mjini Berlin anapompigia simu, Philipp anapata kisingizio cha kukatiza ziara yake. Mama yake Philipp anasikitika sana pale Philipp anapomuaga na kuelekea mji mkuu wa Ujerumani.

Hata kama huna msamiati wa kutosha bado, unaweza kufahamu tukio hili. Maneno ya kimataifa na kiimbo vitakuwezesha kufahamu mtiririko wa tukio na pia kufanya mazoezi ya ufahamu kwa kusikiliza.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa