Tukio 01 – Ziara mashambani (Vijijini) | Radio D Teil 1 | DW | 24.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 01 – Ziara mashambani (Vijijini)

Philipp, ambaye ni kijana, anasafiri kwa gari kwenda mashambani kumtembelea mama yake Hanne. Anatumai kupunga hewa lakini punde anagundua kuwa mashambani pia kuna vitimbi vyake.

Philipp amtembelea mama yake mashambani.

Philipp amtembelea mama yake mashambani.

"Mandhari asilia, raha iliyoje!" Philipp anasema punde anapowasili nyumbani kwa mama yake mashambani, ambako anataka kujipumzisha. Huko kuna zaidi ya paka na ng'ombe. Philipp anapokunywa kikombe chake cha kahawa kwenye bustani, hapati amani aliyoitaraji kwani wadudu wanamsumbua si haba—kisha mambo yanamharibikia Philipp.

Hata kama huna msamiati wa kutosha bado, unaweza kufahamu tukio hili. Sauti zinasosikika chini kwa chini zinaashiria mahali Philipp alipo. Katika tukio hili, utajifunza maamkizi na kauli za kuagana.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa